11 Desemba 2025 - 12:51
Ubalozi wa Iran: Hatua ya Marekani dhidi ya Venezuela ni wizi katika Bahari ya Karibi

Ubalozi wa Iran mjini Caracas, huku ukilaani vikali kitendo cha Marekani cha kukamata mafuta kwenye eneo la karibu na pwani ya Venezuela, umetangaza kuwa hatua hiyo ya Marekani ya kukamata meli ya mafuta ya Venezuela bila sababu yoyote ya kisheria ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni za kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Venezuela, siku ya Alhamisi kupitia tamko rasmi, umeeleza kuwa kukamatwa kwa meli hiyo ya mafuta ya Venezuela katika Bahari ya Karibi ni kitendo kisicho halali, kisicho na msingi wowote wa kisheria, na ni uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa, hususan kanuni ya uhuru wa bahari na haki za meli kusafiri.

Katika tamko hilo imeelezwa:
“Hatua isiyo halali ya serikali ya Marekani ya kukamata meli ya mafuta ya Venezuela bila sababu ya msingi au hoja ya kisheria katika Bahari ya Karibi ni uvunjaji mkubwa wa sheria za kimataifa, ikiwemo kanuni isiyokiukwa ya uhuru wa bahari na usafiri wa baharini. ‘Wizi katika Bahari ya Karibi’ ndilo jina sahihi zaidi kwa kitendo hiki haramu na kisicho na hoja cha Marekani, ambacho kinaonyesha kuwa Marekani inajaribu kutekeleza malengo yake kupitia vitendo visivyo halali, ukiukaji wa mamlaka ya kitaifa ya wengine, na kusambaza vurugu na uanarkia.”

Ubalozi wa Iran: Hatua ya Marekani dhidi ya Venezuela ni wizi katika Bahari ya Karibi

Katika hitimisho la tamko hilo, Ubalozi wa Iran umetangaza mshikamano wake na Serikali na taifa la Venezuela katika kutetea mamlaka yake ya kitaifa na haki zake halali, na kulaani hatua hiyo inayokwenda kinyume na misingi na kanuni za msingi za kimataifa.

Inafahamika kuwa majeshi ya Marekani yaliteka meli moja ya mafuta iliyokuwa chini ya vikwazo, karibu na pwani ya Venezuela.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bloomberg, kukamatwa huko kumetokea wakati ambao Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akitoa matamshi makali zaidi dhidi ya Nicolás Maduro, Rais wa Venezuela, na pia hakutoakanusha uwezekano wa mashambulizi ya ardhini dhidi ya Venezuela.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Venezuela pia kupitia tamko rasmi, imeeleza kuwa kukamatwa kwa meli ya mafuta ya nchi hiyo na majeshi ya Marekani katika maji ya Bahari ya Karibi ni “wizi wa kimataifa wa baharini” na imelilaani kitendo hicho vikali sana.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha